Siku chache baada mwananchi mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mara imetembelea eneo hilo na kutoa maagizo mazito kwa vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo kwa kutaka kukomeshwa mara moja mauaji hayo ya mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya uvamizi wa mgodi wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia Gold Mine.
Akizungumza baada ya kujionea uharibifu mkubwa ambao umefanywa na wananchi katika Kituo cha Afya cha Nyamongo wakati wa vurugu kati ya polisi na wananchi muda mfupi baada mkazi mmoja wa Kijiji cha Mrito kuuawa kwa kupigwa risasi, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mara Magesa Mulongo, amesema haiwezekani wananchi kudai haki kwa kuvunjwa kwa sheria.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuandaa mafunzo maalumu kwa vikundi vya ulinzi wa jadi maarufu kama Seiga kwa kuzingatia sheria za nchi ili vitumike kwa shughuli za ulinzi katika eneo hilo, ambavyo vimekuwa na nafasi kubwa ya kupambana na uhalifu katika eneo hilo.
BOFYA PICHA HAPA CHINI UONE PICHA ZA UCHI BONGO HASA USWAZI
DON'T FORGET TO LIKE THE PAGE IN ORDER TO GET NEWS UPDATES HAPPEN AROUND THE WORLD
Filed Under:
HABARI
on Jumatatu, 16 Mei 2016
Chapisha Maoni