Rais wa Venezuella,
Nicolas Maduro, amesema yuko tayari kuongeza mamlaka yake chini ya
utawala wa hali ya hatari iliyotangazwa wiki iliyopita
.
Hatua hiyo
imefikiwa ili kukabiliana na waandamanaji wanaopinga serikali ya taifa
hilo.Maduro amedai kuwa upinzani unachochea ghasia na pia kupanga njama ya kuipindua serikali yake. Amesema hatasita kuchukua hatua zinazofaa ili kudumisha amani nchini Venezuela, ambayo inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi.
Chanzo BBC.
Chapisha Maoni