Magoli ya Simon Msuva na Matheo Anthony yameiweka yanga kwenye mazingira mazuri ya kufuzu kucheza hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Yanga wamepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sagrada Esparanca ya Angola, magoli yote yakifungwa kipindi cha pili cha pambano hilo.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka suluhu lakini Yanga wakiwa wametengeneza nafasi kadhaa wakashindwa kuzitumia kupata ushindi wa mapema. Esparanca walifanikiwa kuibana vizuri Yanga kipindi cha kwanza kwa kuwanyima nafasi washamulizi Amis Tambwe na Malimi Busungu walioanza pamoja kwenye mchezo huo.
Benchi la ufundi la Yanga lilifanya mabadiliko kwa kuwaningiza Mbuyu Twite, Geofrey Mwashiuya na Matheo Anthony ambao walibadilisha kasi ya mchezo na kufanikiwa kupata ushindi huo muhimu kwao kwenye uwanja wa nyumabani.
Simon Msuva alianza kuifungia Yanga bao dakika ya 71 kipindi cha pili kwa kuunganisha kwa kichwa krosi ya Geofrey Mwashiuya kabla ya kabla ya Matheo kuipa Yanga bao la pili dakika za nyongeza kwa shuti kali akiwa nje ya takribani mita 25 kutoka golini.
Chapisha Maoni